">

Friday, June 24, 2011

Katika uwembamba na wepesi "dell laptop hii ni zaidi"

Dell Latitude Z600 laptop
Miongoni  mwa matoleo ya laptop mpya  za dell,Z600 Laptop ndio pekee ilivunja rekodi ya kuwa laptop nyembamba na nyepesi zaidi katika zaidi ya miaka miwili mpaka sasa,ina uzito wa 4.4 lbs sawa na 1.995806428 kilograms(2 kgs),na wembamba wa nusu" inch".uwezo wake ina Intel Core 2 Duo 1.6 processor pamoja 4.0 GB DDR integrated memory, SSD drive, Wi-Fi connectivity, 16" high definition LCD display pia 2MP autofocus web-cam.
Dell latitude Z600 laptop ikiwa kwenye chaji stand yake inayotumia teknologia ya wireless....upoooo?
Lakini sifa ya kipekee katika  laptop hii imekuja na chaji ya dizaini yake ni ya stand ambayo inatumia mfumo wa "wireless" yawezekana ndio laptop pekee kutumia na mfumo huu.

Usiogope bei,waswahili husema kizuri gharama ,inauzwa kuanzia dola za kimarekani 2,000  inategemeana na uwezo wake....ciao

Fahamu yanayojiri katika ulimwengu wa Teknologia

JAPAN  Waongoza kwa kutengeneza kompyuta kali zaidi duniani.
  • Katika listi ya kompyuta 500 bora zenye kiwango cha ubora na uwezo wa juu zaidi duniani iliyotolewa hivi karibuni,imeonyesha kuwa kuna mabadiliko mengi yaliyofanyika.
  • Baada ya kutolewa kwenye chati mwaka 2004,Japan hivi sasa wamerudisha heshima yao na kurudi tena kileleni  kwa kufyatua " top-performing supercomputers in the world".Chati ya hivi karibuni ya kompyuta 500  bora imeonyesha muundo wa kwanza uliyoongoza mpaka hivi sasa unaoitwa K Computer,uliotengenezwa katika taasisi moja ijulikanayo kwa jina la RIKEN Advanced Institute for Computational Science iliyopo mjini Kobe.
  •  Muundo wa K Computer una uwezo katika utendaji zaidi " 8 quadrillion calculations per second (petaflop/s)".(hii ni processor zenye kiwango cha juu duniani zinazotengezwa na  kampuni ya intel)


    Muundo mpya wa K Computer uliotengenezwa na RIKEN Advanced Institute for Computational Science ndio  "world’s most powerful supercomputer "mpaka sasa.

    Chati hii ya ubora hutolewa mara mbili kwa mwaka iliyoidhinishwa na baraza lijulikanalo kama "the annual U.S. and international supercomputing conferences"

    kufuatilia chati hii ya kompyuta zenye ubora na uwezo zaidi duniani tembelea wavuti hii; www.top500.org