">

Friday, June 24, 2011

Fahamu yanayojiri katika ulimwengu wa Teknologia

JAPAN  Waongoza kwa kutengeneza kompyuta kali zaidi duniani.
  • Katika listi ya kompyuta 500 bora zenye kiwango cha ubora na uwezo wa juu zaidi duniani iliyotolewa hivi karibuni,imeonyesha kuwa kuna mabadiliko mengi yaliyofanyika.
  • Baada ya kutolewa kwenye chati mwaka 2004,Japan hivi sasa wamerudisha heshima yao na kurudi tena kileleni  kwa kufyatua " top-performing supercomputers in the world".Chati ya hivi karibuni ya kompyuta 500  bora imeonyesha muundo wa kwanza uliyoongoza mpaka hivi sasa unaoitwa K Computer,uliotengenezwa katika taasisi moja ijulikanayo kwa jina la RIKEN Advanced Institute for Computational Science iliyopo mjini Kobe.
  •  Muundo wa K Computer una uwezo katika utendaji zaidi " 8 quadrillion calculations per second (petaflop/s)".(hii ni processor zenye kiwango cha juu duniani zinazotengezwa na  kampuni ya intel)


    Muundo mpya wa K Computer uliotengenezwa na RIKEN Advanced Institute for Computational Science ndio  "world’s most powerful supercomputer "mpaka sasa.

    Chati hii ya ubora hutolewa mara mbili kwa mwaka iliyoidhinishwa na baraza lijulikanalo kama "the annual U.S. and international supercomputing conferences"

    kufuatilia chati hii ya kompyuta zenye ubora na uwezo zaidi duniani tembelea wavuti hii; www.top500.org


No comments:

Post a Comment